Msichana iniative, ni Taasisi isiyo ya Kiserikali
inayojishughulisha na kuwatetea watoto wa kike katika masuala mbali mbali. Hivi
karibuni Taasisi hiyo ilifungua kesi ya Kikatiba yenye lengo la kupinga sheria
ya Ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu mtoto wa kike aolewe akiwa na miaka 15.
Katika kesi hiyo Msichana Iniative iliomba Mahakama Kuu itamke kwamba msichana
kuolewa chini ya mika 18 ihesabike ni kosa.
Mahakama Kuu ilikubaliana na ombi la watetezi hao na kutamka
kuwa ni kosa binti kuolewa akiwa na
miaka 15, huku makahakama hiyo ikiipa Serikali mwaka mmoja kurekebisha
mapungufu hayo yaliyomo katika sheria hiyo kwa kutamka kwamba umri sahihi wa
kufunga ndoa ni miaka 18 kwa wote wavulana na wasichana.
Imeripotiwa kwamba Serikali ya Tanzania inakusudia kwenda
Mahakamani kukata rufaa ya hukumu hiyo. Yaani ni kama Serikali inasema umri huo
wa miaka 15 ni sahihi. Lakini swali linaloumiza kichwa ni kwamba ikiwa umri huo
ni halali ni kwanini mtoto mwenye umri huo huo asiruhusiwe kupiga kura hadi
afikishe miaka 18 wakati tendo la kura ni la muda tu na ndoa ni ya kudumu?
Sheria za Tanzania, zinatambua kwamba mtu mwenye umri wa
miaka 15 ni mtoto asiyeruhusiwa hata kupiga kura. Lakini pia anahesabika kuwa
yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake.
Waislamu Tanzania wanasema sheria hiyo inayotamka kwamba msichana
aolewe hata akiwa na miaka 15 ilitungwa kutokana na ushauri wa wazee wa
Kiislamu wakiongozwa na Sheikh Marehemu Muhammad Ali al Bukhri wakati wa
kutunga sheria hizo.
Kwa muda mrefu sheria hiyo imepigiwa sana kelele na asasi mbali
mbali zikiipinga sheria hiyo kwa kuiona inakiuka haki za binadamu ikiwemo
kumnyima elimu binti anayetamani kusoma kwa kuruhusu wazazi wake kumuoza hata
akiwa na miaka 15 tu.
Swali kubwa linalojitokeza ni kwamba ni kwa nini baada ya
hukumu hiyo kutolewa vyombo vya habari vya Kiislamu vya hapa Tanzania
vinailalamikia sheria hiyo kwa kuiita hujuma dhidi ya Uislamu?
Wanasema, “ si haki kuigusa sheria nyeti kama hiyo bila kushirikisha wadau wote, jambo
walilolitafsiri kuwa ni sawa na kuihujumu sheria ya ndoa ya Kiislamu.”
Katika Uislamu mmoja wa wake za Mohammad aitwaye Bi Aysha
aliolewa na Mtume wa Waislamu Mohammad akiwa na miakla 6 huku yeye Mohammad akiwa
na miaka 53 na akaanza kushiriki naye tendo la kujamiiana naye akiwa ana miaka
10 huku Mohammad akiwa na miaka 57.
Kwa hiyo sharia za Kiislamu zilizotolewa kupitia ushauri wa
wazee wa Kiislamu kuhusiana na suala nyeti la ndoa ndilo limekuwa kikwazo cha
mabadiliko ya haraka ya sheria hiyo kandamizi dhidi ya wasichana.
Serikali kila wakati imekuwa ikishauriwa kuibadilisha siku
ya Jumapili kutoifanya siku ya kupiga kura kwa sababu ni siku ya ibad kwa
baadhi ya Wakristo, mpaka leo imegoma, lakini inaonekana iko tayari kwenda
makahama kuu kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kwa lengo la kutetea
maslahi ya Uislamu badala ya maslahi mapana ya taifa.
Daniel Mwankemwa
Dar es Salaam
04 Agosti, 2016
Dar es Salaam
04 Agosti, 2016
0 comments:
Post a Comment