Translate

Wednesday, April 14, 2010

JE NI WAISLAMU TU NDIYO WANAOTAKIWA KUCHINJA WANYAMA KWA AJILI YA CHAKULA?

UCHINJAJI WA WANYAMA: NI NANI ALIYEWAPA RUKSA WAISLAMU PEKE YAO KUCHINJA WANYAMA?
Kumekuwa na tatizo linaloisumbua jamii yetu linalohusiana na uchinjaji wa nyama tunayotaka kuitumia watu wa imani na dini mbalimbali. Kwa bahati mbaya sana kuna kundi moja la kiimani (Waislamu) wao ndiyo hujipa haki hiyo zaidi na imefikia hatua ambayo hutaka kusababisha uvunjifu wa amani pale wanapoona watu wengine pia wasio wa imani yao wanapochinja mnyama huwaita makafiri na chakula chao ni haramu. Je ni kweli?

Uislamu umeanza 610 B.K wakati huo dini zingine kama Uyahudi , Ukristo kwa kuzitaja kwa uchache zilikwisha kuwapo. Je hao walikuwa hawali nyama? Na kama walikuwa wanakula walikuwa wanachinjiwa na nani Waislamu wakiwa hawapo? Nani aliyekuja kutangaza baadaye kuwa ni Waislamu tu ? Je ni serikali?

Kwa muda mrefu Waislamu wamekuwa wakijaribu kuishawishi Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itunge sheria moja itakayoitambua dini moja tu ya Kiislamu ndiyo ihusike na uchinjaji wa wanyama kwa ajili ya matumizi ya Watanzania wote.

Hoja ya namna hiyo iliwahi kupelekwa katika kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mh. Hafidh Ali Tahir, Mbunge wa CCM, Dimani, Zanzibar, katika Mkutano wa Tano, Kikao cha Tano cha Bunge , cha tarehe 6 Novemba,2009 kama alivyonukuliwa na Taarifa Rasmi ya Bunge, (HANSARD),uk.55,56 ninamnukuu “ Sasa Mheshimiwa Waziri, ningemwomba basi akaangalia na sehemu zote hizi mbili. Sitaki aende ndani sana lakini ninachosema ni kwamba bodi ifike mahali iweke sheria, kuwe na kanuni ya uchinjaji wa nyama ambao tunataka tuwatumie. Tusichinje tu. Ndiyo nikasema kwamba Tanzania haina dini lakini Watanzania wana dini, tunakula kula nyama hii. Sasa kuwe na utaratibu maalumu. Sasa Mheshimiwa Waziri, hili atakuja kutuambia vipi angalau basi tuweke utaratibu unaofahamika. (Makofi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakupa mfano ukienda nchi za wenzetu hasa nchi za Kiarabu, si kwamba wote watakuwa Waislamu kwa sababu ni nchi za Kiarabu hapana. Ndani ya nchi za Kiarabu kuna watu wana dini nyingine na wala usije ukasikia mtu anaitwa Hafidh Al-Saad kwa mfano, ukafikiria ni Muislamu,hapana ni jina tu hilo. Lakini dini yake ikawa nyingine. Abdulaziz utasema kwa jina hili huyu Muislamu hapana si Muislamu jina kitu kingine dini kitu kingine. Sasa wenzetu kwa sababu ya kuweka tofauti pale ambapo kunachinjwa nyama halali, basi unapokwenda katika ranchi yao ya kuchinjia kile kisu kimeandikwa Bismillah na kule alikoelekea yule ng’ombe ndiko kunakokubalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyama zinauzwa Dar es Salaam, Dodoma na mahali pengine,wallah hawaulizwi kwenye bucha wamechinja wapi nyama hiyo, hawaulizi wala hawaulizwi kwamba ngombe huyo alivyochinjwa kaelekea Kibla, sote tunakwenda kununua nyama, tunaondoka. Lakini nasema lazima kama ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunataka kupitisha jambo hili lazima tuwe na tahadhari. Sasa namwomba Mheshimiwa Waziri awe na tahadhari na hili mbaya hajitokezi sasa anajitokeza baadaye” Mwisho wa kunukuu

Hilo ndiyo ombi lililopelekwa Bungeni ili Bunge litunge sheria ya namna ya uchinjaji wa nyama. Mh. Hafidh Ali Tahir alipendekeza sheria itakayotungwa lazima izingatie zaidi utaratibu wa Kiislamu akimaanisha wanyama wanapochinjwa wachinjwe kwa kuelekezwa Kibla, uelekeo ambao Waislamu huelekeza nyuso zao wakati wa kufanya ibada zao, yaani Makka.

Waziri wa Mifugo wa kipindi hicho Mh. Anthony Diallo (MB) akijibu ombi hilo alitoa msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kuhusu uchinjaji. Ninamnukuu kama alivyonukuliwa katika uk.88 wa Hansard hiyo hiyo ya Bunge.

Anasema “ Kwa hiyo, muuzaji nyama yeyote ni lazima atazingatia kitu ambacho ni desturi na mila na matakwa ya wanunuzi wa nyama hiyo. Kwa hiyo, hatuhitaji kuweka kwenye sheria kwa sababu tunafahamu Serikali yetu haina dini na hatuwezi kuanza kuingiza vifungu vya kutamka mahitajio ya dini moja au dhehebu moja ndani ya sheria tunakiuka Katiba ambayo inatukataza Serikali isijihusishe na uhuru wa dini ni wa kila mtu sio wa Serikali”. Mwisho wa kunukuu.

Qur’an nayo inayaeleza makundi yanayotakiwa kuchinja na chakula hicho kiwe halalai kwa Waislamu. Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maidah, 5:5 “ Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na chakula cha wale waliopewa kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao……..”

Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu waliopewa kitabu ni Wayahudi na Wakristo (Manasara).

Unaposoma ufafanuzi wa aya hiyo ndani ya Qur’an unasema “Chakula cha kuchinja hakiwi halali kwa Mwislamu ila kichinjwe na (a) Mwislamu (b) Myahudi (c) Mnasara (Mkristo) Kwa sharti ile ya kuchinja siyo kuwanyonga”

Hivyo mbali na Mwislamu, Myahudi na Mkristo pia wanayoruhusa kuchinja na Mwislamu akala bila hofu yoyote.

Muislamu anaweza kuchinja mnyama hata kwa kutamka jina lake tu akisahahu kutamka jina la Mwenyezi Mungu. Mkweli Mwaminifu, kimeandikwa na Sheikh Said Moosa Mohammed al-Kindy wa Muscat Oman, Juzuu 3-4, uk.13 Hadith na.727 inasomeka hivi: Muislamu inamtosheleza jina lake,basi akisahau kusema jina (la Mwenyezi Mungu) wakati anapochinja, basi aseme (anapokumbuka) kisha ale”.

Je jina la muislamu huyu lina uhalali gani hata kuwafanya wengine wale vibudu

Hata vitabu mbali mbali vinaeeleza kuwa Chakula cha Wakristo ni halali pia hata kwa Waislamu Safari moja aliulizwa Abu Dardaa (r.a) kuhusu beberu aliyechinjwa kwa ajili ya kanisa linaloitwa Jurjus:- Utakula nyama yake? Akajibu Abu Dardaa, Ewe Mola naomba msamaha, wao ni watu wa Kitabu chakula chao ni halali kwetu na chetu ni halali kwao.” Akaamrisha aliwe.

Katika uk.71 wa Kitabu hicho hicho cha Halal na Haram kinaendeleza kueleza: Kanuni ; Tusilo Tusiloliona. Wala si juu ya Muislamu kuuliza mambo asiyoyaona. Vipi kimechinjwa? Je, shuruti za kuchi nja zimekamilika ? Je, limetajwa jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinja au halikutajwa? Haya si ya kuulizwa, bali kanuni ni kuwa kila kilichochinjwa an Muislamu-hata akiwa jahili au fasiki- au kilichochinjwa na Myahudi na Mkristo, maadamu hatukukiona kilivyochinjwa basi ni halali kukila”. Mwisho wa kunukuu.
Safari moja aliulizwa Abu Dardaa (r.a) kuhusu beberu aliyechinjwa kwa ajili ya kanisa linaloitwa Jurjus:- Utakula nyama yake? Akajibu Abu Dardaa, Ewe Mola naomba msamaha, wao ni watu wa Kitabu chakula chao ni halali kwetu na chetu ni halali kwao.” Akaamrisha aliwe.

0 comments:

 
Powered by Blogger