Translate

Tuesday, September 14, 2010

HIVI RAIS WETU NI MSHIRIKINA?

SHEIKH YAHAYA NI MCHAWI NA MSHIRIKINA. MWEZI MACHI MWAKA HUU NILIALIKWA NA KITUO CHA REDIO WAPO KATIKA KIPINDI CHAKE MAARUFU CHA MEZA YA BUSARA ILI KUONGELEA SUALA HILI LA UNAJIMU WA SHEIKH YAHAYA, NA HASA BAADA YA YEYE KUTANGAZA KWAMBA ATAKAYEMPINGA RAIS KIKWETE KATIKA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS KATIKA CHAMA CHA CCM ATAKUFA.

NILIIWASILISHA MADA HIYO . KWA UPANDE WA WAISLAMU ALIALIKWA USTAADH SULEYMAN MBOGO ILI AELEZE UISLAMU UNASEMA NINI KUHUSU AINA YA WATU KAMA AKINA SHEIKH YAHAYA NA UNAJIMU WAO.

 USTAADH SULEYMAN ALIWAAMBIA WASIKILIZAJI WA KIPINDI HICHO KUWA NI USHIRIKINA KUJIHUSISHA NA MAMMBO YA UNAJIMU. MWENDESHA KIPINDI HICHO AMBAYE NI MTANGAZAJI WA REDIO WAPO FM NDUGU SABINUS MBOGO ALIOMBWA NA WASIKILIZAJI KUWA ASIHITIMISHE MADA HIYO MPAKA ATAFUTWE SHEIKH YAHAYA MWENYEWE TUWE NAYE PALE STUDIO TUMUULIZE MASWALI KWA MUJIBU WA IMANI ZETU NA YAKE KUHUSU HUO UNAJIMU WAKE. ALISEMWA ANAUMWA NA MPAKA LEO HAJAKWENDA REDIO WAPO.

 NILIAMUA KUANDAA SOMO LINALOHUSU UNAJIMU WA NYOTA KATIKA DINI YA UISLAMU NA UKRISTO BAADA YA KUONA SHEIKH HUYO AKIHUSISHA NYOTA ILIYOJITOKEZA ALIPOZALIWA YESU NA AINA YA UNAJIMU WAKE, AMBAYO MPAKA SASA INAENDELEA KUCHAPISHWA KILA WIKI KATIKA GAZETI LA KIKRISTO LA NYAKATI LIKIWA KATIKA TOLEO LA TANO WIKI HII. (TAFUTA NAKALA HIZO TOKA 1-5)

KATIKA MAKALA HIYO NILIMTAJA KWA JINA SHEIKH YAHAYA KUWA YEYE NI MJUMBE WA IBILISI NA SHETANI KWA AJILI YA HIZO KAZI ZAKE NA NILIMUULIZA MASWALI MAGUMU KUHUSU CHANZO CHA UNAJIMU WAKE AMBAYO MPAKA LEO HAYAJAJIBIWA.NILIJUA HAWEZI KWA SABABU MUNGU ALIKWISHA WAKATAA WANAJIMU TANGU NYAKATI ZA MFALME NEBKADREZA (DAN 2:26) WA BABELI.

 NINAPOONA USHIRIKINA HUO HATA RAIS WANGU ANAHUSISHWA KWA MARA NYINGINE TENA BILA YEYE BINAFSI KUKANUSHA,INA MAANA YOTE SHEIKH YAHAYA ANAYOSEMA KUMHUSU RAIS WETU, RAIS MWENYEWE ANAYAAMINI, WAKATI CHANZO CHA UNAJIMU WAKE NI MAJINI (MASHETANI)?

 NINAMUOMBA RAIS WANGU AMJIBU SHEIKH YAHAYA YEYE MWENYEWE BILA KUWAACHIA WASAIDIZI WAKE KWA MAANA JAMBO HILI NI LA BINAFSI SANA. RAIS AKIJIBU NITATOA SOMO KUHUSU HAYO MAJINI NA HUO UNAJIMU KUWA NI NINI. HIVI RAIS WETU NI MSHIRIKINA?

0 comments:

 
Powered by Blogger