Translate

Tuesday, April 6, 2010

WAISLAMU WANASEMA HAKUNA PASAKA

Wakristu Duniani kote Tarehe 4 pril tumesherehekea Kufufukwa kwa Yesu Kristo Mkombozi wetu, Sherehe ambazo ni alama kuu au kumbukumbu kuu ya ushindi dhidi ya Shetani. Kwa bahati mbaya sana ndugu zetu Waislamu kwa miaka yote wamekuwa wakipinga na kujaribu kupindisha ukweli huu, wamekuwa wakitumia mihadhara, magazeti na tovuti kufanikisha upotoshaji huo. Na hivi karibuni tulipokuwa tukikaribia sherehe hizi gazeti moja la Kiislamu liitwalo Mapenzi ya Mungu toleo Na. 159 liliandika habari ya upotoshaji ikiwa na kicha cha habari PASAKA KATIKA NYAYO ZA UPAGANI. Mengi wameandika, lakini yote katika upingaji na upotoshaji. Waislamu wamekuwa wakitumia aya wasizozielewa kutoka katika Maandiko Matakatifu kwa ajili ya kupotoshea, na wamekuwa wakitumia maandiko yao pia kupotoshea.

Hoja za Waislamu

Quran Suratul Nissaa, (Wanawake) 4:157
Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa (Yesu), mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsulubu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.
===
Quran inapinga kifo cha Yesu na hapo hapo inataka watu waamini kuwa aliyesulubiwa na kufa hakuwa Yesu
===

Waislamu wanatumia aya zifuatazo hapa chini kujaribu kuwafanya watu waamini kwamba Yesu mwenyewe alisherehekea Sikukuu ya Pasaka bila kuelewa kuwa Aya hizo zinahusiana na Pasaka ya Wayahudi ambayo ndio msingi wa pasaka yetu ya leo ambayo ni Yesu kristo mwenyewe.

Yoh 2:13 Ilipokaribia wakati wa Pasaka ya Wayahudi, Yesu alipanda kwenda Yerusalemu.

Yoh 6:4 Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.

Yoh 11:55 Basi Pasaka ya Wayahudi ilipokuwa imekaribia, watu wengi walitoka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajitakase.

Mat 26:17 Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate isiotiwa chachu wale wanafunzi walikuja kwa Yesu wakamwuliza, ``Ungependa tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?''

Luka 22:7-8. 7Ikafika siku ya Mikate isiyotiwa Chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. 8Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza, ``Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.


Pasaka ya Wayahudi

Kut 12: 21 Ndipo Mose akawaita wazee wote wa Israeli na kuwaambia, ‘‘Nendeni mara moja mkachague wanyama kwa ajili ya jamaa zenu mkachinje mwana kondoo wa Pasaka.

Kut 12:5 Kila mwanamume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, aketiye penye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mtumwa wa kike, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo.

Kut 12:8 Usiku huo huo watakula nyama iliyookwa kwenye moto, pamoja na mboga chungu za majani na mikate isiyotiwa chachu.

== == ==
Aya zilizooneshwa hapo juu zinajulisha kuwa Pasaka ya Wayahudi walitumia mnyama mwenye miguu minne, mkate usiotiwa chachu, na mboga chungu
== == ==

PASAKA YA KIKRISTO- NI YESU KRISTO MWENYEWE

1 Kor 5:7-8 7Ondoeni chachu ya zamani ili mpate kuwa donge lisilo na chachu, kama mnavyotakiwa kuwa. Kwa maana Kristo ambaye ndiye Mwana-kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kama dhabihu. 8Kwa hiyo, tusherehekee sikukuu hii, sio kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu bali kwa mkate usiotiwa hamira, wa moyo safi na kweli

Yoh 1:29 Kesho yake Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, ``Tazameni! Huyu ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu anayeondoa dhambi ya ulimwengu!

Ufunuo 5:8-9. 8Alipokwisha kuichukua ile hati, wale viumbe wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ubani , ambao ni maombi ya watu wa Mungu. 9Nao wakaimba wimbo mpya: ``Wewe unastahili kuichukua hati na kuifungua mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila na kila lugha; watu wa kila jamaa na kila taifa.

Mat 26:26-28. 26Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, ``Chukueni mle; huu ni mwili wangu.'' 27Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa akisema, ``Kunyweni nyote katika kikombe hiki. 28Hii ni damu yangu ya agano ambayo inamwagika kwa ajili ya wengi ili wasame hewe dhambi.

Luka 22:14-20 14Wakati ulipofika Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 15Kisha akawaambia Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu 17Akapokea kikombe cha divai akashukuru, akasema, ``Chukueni mnywe wote. 18Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja. 19Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi. 20Vivyo hivyo baada ya kula, aka chukua kile kikombe cha divai akasema, ``Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.

= = =
Pasaka katika Agano Jipya, Yesu ndiye Mwanakondoo mwenyewe wa Pasaka asiye na ila wala waa

= = =
Muda wa kufa kwa mwanakoondoo wa Pasaka, Yesu

Katika Agano la Kale mwanakondoo alitakiwa kuchinjwa jioni
Kut 12:6 Tunzeni wanyama hao mpaka siku ya kumi na nne ya mwezi, ambapo lazima watu wa jumuiya yote ya Israeli wachinje wanyama hao wakati wa jioni..

Katika Agano Jipya mwanakondoo aliuwawa jioni ili kutimiza taratibu za Pasaka
Mat 27: 45-50. 45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza. 46Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, ``Eli, Eli lama sabakthani?'' Yaani, ``Mungu wangu, Mungu wangu, mbona ume niacha?'' 47Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, ``Anamwita Eliya!'' 48Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo moni. 49Lakini wengine wakasema, ``Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.'' [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni, pakatoka maji na damu]. 50Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho.

Marko 15:33-37 33Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu ``Eloi, Eloi lama Sabaktani?'' Yaani, ``Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?'' 35Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, ``Mnamsikia? Anamwita
36Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, ``Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!''
37Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.
Luk 23:44-47. 44Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa, 45kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46Yesu akapaza sauti akasema, ``Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.'' Baada ya kusema haya, akakata roho.
47Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, ``Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.''
Mat 1:21 Naye atamzaa mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yesu; kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.''

Ebr 9:11-14 11Kristo alipokuja kama kuhani mkuu wa mambo mema ambayo tayari yamekwisha wasili, alipitia kwenye hema ya kuabudia ambayo ni kuu zaidi na bora zaidi na ambayo haikujengwa na binadamu, yaani ambayo si sehemu ya ulimwengu huu ulioumbwa. 12Yeye aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa wakati wote, akichukua, si damu ya mbuzi na ndama, bali damu yake mwenyewe, na hivyo kutupatia ukombozi wa milele. 13Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama hunyunyizwa juu ya watu wachafu kidini ikawatakasa kwa kuwaondolea uchafu wao wa nje, 14damu ya Kristo ambaye kwa njia ya Roho wa milele alijitoa mwenyewe kwa Mungu kama sadaka isiyokuwa na doa, itazisafisha dhamiri zetu zaidi sana kutokana na matendo yaletayo kifo, na kutuwezesha kumtumikia Mungu aliye hai.

Ebr 9:24-26 24Kwa maana Kristo hakuingia kwenye hema ya kuabudia iliyotengenezwa na bina damu kama mfano wa hema halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ambapo sasa anatuwakilisha mbele za Mungu. 25Wala hakuingia mbinguni kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama kuhani mkuu ain giavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka na damu ambayo si yake. 26Ingekuwa hivyo, ingalimpasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini ilivyo ni kwamba ametokea mara moja tu kwa wakati wote, katika siku hizi za mwisho, ili atokomeze dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu.
Ebr 10:8-10 8Kwanza alisema, ``Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa wala sadaka zitolewazo kwa ajili ya dhambi hukutaka, wala huku pendezwa nazo,'' ingawa hizi zilitolewa kwa mujibu wa sheria. 9Kisha akasema, ``Niko hapa, nimekuja kutimiza mapenzi yako.'' Anaweka kando ule utaratibu wa kwanza na kuanzisha utaratibu wa pili. 10Na kwa mapenzi hayo, sisi tumetakaswa kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu, kwa wakati wote.

== == ==
Waislamu huamini kuwa Isa a.s ndiye Yesu Kristo, jambo hilo halina ukweli wowote. Endelea kufuatilia kibaraza hiki ili kujua utofauti wao

2 comments:

John Mwaipopo said...

mimi nafikiri tuwaache tu kwa kuwa hawakukata japo kidole chetu.

Anonymous said...

penye ukweli uongo ujificha.

 
Powered by Blogger