Karibuni kwenye uwanja wa mafundisho sahihi yanayoweza kukusaidia kujua njia ya kweli ya kumfikia Mwenyezi Mungu. Mungu aliweka njia moja inayotakiwa kufuatwa na wanadamu wote ili waweze kufika kwake. Hata hivyo, wanadamu kutokana na nguvu wasizozielewa wamevumbua njia zao wenyewe. Fuatilia Blog hii ili upate ukweli , na ukweli wala si vinginevyo, kutokana na kuwa ilishatabiriwa kuwa kutakuwa na upotoshaji juu ya ukweli wa neno la Mungu na njia sahihi ya kumfikia Yeye, kama tunavyoona katika Maandiko Matakatifu ya Biblia.
"Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa; vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; Katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewana nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe. Basi, wapenzi mkitangulia kuyajua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuacha uthibitifu wenu".
0 comments:
Post a Comment