Utangulizi : Siku zote Mkristo Mwana wa Mungu ,anapomuelezea Mungu katika ukuu na uwezo wake,kwa wale wasioamini hususani Waislam na Mashahidi wa Jehova (Jehova’s Witness), na akamtaja Mungu huyo kuwa ni Mungu katika Utatu Mktakatifu, huzuka malumbano au mabishano kuhusu jambo hilo. Mashahidi wa Yehova husema wale wanaomini katika Utatu Mtakatifu wamefuata imani za kipagani kwa sababu katika Biblia nzima hakuna mahali popote palipoandikwa Utatu Mtakatifu upinzani huo huandikwa mara kwa mara katika vijarida mbali mbali .
Hoja kuu kuwahusu ni kuwa siku zote hawapendi kukupa nafasi uwaelekeze kwa nini unasema hivyo , bali wakati wote hukutaka uoneshe neno “Utatu Mtakatifu “ ndani ya Biblia. Na kwa hakika hupati neno hilo “ Utatu Mtakatifu” ndani ya Biblia .
Swali la ufahamu : Je kukosekana neno UTATU MTAKATIFU ndani ya Biblia kama wanavyodai mashahidi wa Yehova kuna mfanya Mungu asiwe wa Utatu ? Jibu la swali hili ni rahisi sana SI KWELI. Hii ni kwa sababu, kuna maneno ambayo hayapo ndani ya Bblia yakimhusu Mungu, lakini yatumikapo huleta maana nzuri na yenye uhakika kuhusu yeye Mungu .Maneno hayo yanapotamkwa kwa lugha ya kigeni ni Omnipotence yaani Mungu ni mwenye nguvu zisizo shindikana na chochote , Omnipresence yaani Mungu yupo mahali pote kwa wakati wote na Omniscience yaani Mungu anajua yote maneno haya yaani Omnipotence , Omnipresence na Omniscience hayajaandikwa katika Biblia ya lugha ya Kiingereza, lakini yatamkwapo hueleza jambo la maana na lenye umuhimu kumhusu Mungu. Ndivyo ilivyopia kwa neno “Utatu Mtakatifu” yaani Trinity”
Waislam wao hupinga utatu mtakatifu kwa kujaribu kusoma baadhi ya aya zilizomo ndani ya Quran, kitabu kinachoongoza imani yao hasa pale wanaposema katika Suratul Al- Maidah,(meza), 5:73 “Kwa hakika wamekufuru wale waliosema mwenyenzi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu (yeye ndiye watatu wao ) hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja ( tu peke yake) na kama hawataacha hayo wasemayo kwa yakini itawakamata wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao adhabu iumizayo”.
Unaposoma ufafanuzi wa aya hiyo ya 73 iliyomo ndani ya Qurani hiyo hiyo unasema “unatajwa ukafiri wa kinasara (Ukristo) kwa itikadi zao zote tatu kuwa Nabii Issa (a) Mungu au (b) Mtoto wa Mungu au (c) Mmoja katika waungu hao watatu “yeyote katika itikadi hizi ni ukafiri usiokuwa na shaka na jaza yake ni moto tu”
Pengine jambo linalowasumbua waislam ni ukosefu wa ufahamu kuwa siku zote wanapomfikiria Issa kuwa ndiye Yesu wanapotoka sana .Hii ni kwa sababu Issa siye Yesu na tunatambua hayo hasa tunaposoma vitabu vya kiislam vilivyoandikwa na wanazuoni (wasomi ) wakubwa wa kiislam. Kwa mfano katika Qurani ya Tafsiri ya Imam Baidhwaw, juzuu 1 uk 160 ,anasema Issa maana yake ni wekundu unaozidiana na weupe, na wengine husema Issa maana yake ni dume la ngamia .Hoja hizi zinaungwa mkono na hadithi mbalimbali za kiislamu, zinazomzungumzia Issa, hasa ile inayopatikana katika Sahihi Bukhari Juzuu 4 Hadithi 653, na katika Al-lulu wal- Marjan,kitabu cha 3 Hadithi na 1528 uk.883 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema “Issa Ibn Mariam (a,s) alimwona mtu anaiba akamuuliza !umeiba? akasema hapana ,Naapa kwa Allah ambaye hakuna mola isipokuwa yeye .Issa (a.s) akasema nimemuamini Allah na limeniongopea jicho langu”.
Huyu Issa hawezi kuwa ndiye Yesu kwa sababu Yesu anayajua yote hahitaji kuelezwa na mtu .Katika Injili ya Yohana 1:47-48 “ Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona”
Hivyo maelezo yaliyomo katika Quran pamoja na vitabu vya hadithi za kiislam yana thibitisha kuwa Issa siyo Yesu kwa sababu jina Yesu ni sawa na jina la kiebrania Yehshua ambalo maana yake Mwokozi Math 1: 21, Lk 2: 10- 11. Pia Yesu aliyajua yote hata yaliyomo katika mioyo ya watu hata bila ya wao kusema Marko 2: 8 , Yoh 1: 48-50 tofauti na Issa ambaye hajui jambo lolote na kwa mujibu wa Quran na hadithi zake Issa atahukumiwa kwenda Jehanamu ya moto (Suratul Anbiyaa, (manabii) 21:98, na 5:116-117). Kwa msaada zaidi wa kujua tofauti ya Issa na Yesu agiza kwetu somo hili tunalo.
Hoja wanazotumia mashahidi wa Yehova kupinga fundisho la utatu.
Math 4: 1 “ Yesu alijaribiwa na Ibilisi”
Yakobo 1: 13 “ Mungu hajaribiwi “
Yoh 8: 40 “ Yesu alisema mimi mtu”
Yoh 17: 3 “ Yesu alisema wakujue wewe mungu wa pekee.
I Tim 2: 5 “ Yesu ni mwanadamu tu ( siyo Mungu)
Pia unaposoma katika jarida litolewalo na Mashahidi wa Yehova liitwalo ‘Je Tuamini Utatu” ule uk 20-23 linaelezea kuwa “Roho Takatifu (Na siyo Roho Mtakatifu ) huonyesha kwamba ni kani yenye kudhibitiwa ambayo Yehova Mungu hutumia kutimiza makusudi yake ya namna mbalimbali. Kwa namna fulani, yaweza kufananishwa na nguvu za umeme , kani ambayo yaweza kutumiwa kwa njia tofauti ili iendeshe mambo kwa hiyo Roho Takatifu si mtu na si sehemu ya utatu , wala si sehemu ya Uungu.
Tunapoangalia uislam na waislamu, wao kwao, Roho Mtakatifu ni malaika maarufu katika dini hiyo aitwaye Jibril. Katika Suratul Al- Bagarah (ng’ombe jike) 2:87 “Na hakika tulimpa Musa kitabu na tukawafuatisha mitume (wengine) baada yake na tukampa Issa mwana wa Mariam hoja zilizo wazi wazi na tukamtia nguvu kwa roho takatifu (Jibril)---------------“
`Unaposoma ufafanuzi wa aya hiyo ya 87 ndani ya Quran unasema
“Kwa waislam Roho Mtakatifu ni malaika Jibril si yule wanayedai Wakristo kuwa ni mmoja wa asili ya Utatu (Trinity).
Kwa ufafanuzi huu Wasomi wa Kiislamu wanajua kuwa namna fundisho la Utatu Mtakatifu tunavyolizungumza sisi Wakristo kwa mujibu wa Biblia Takatifu, ni tofauti kabisa na vile watu wengine wasio Wakristo wanavyolizungumzia fundisho hilo wakiwemo Waislamu na Mashahidi wa Yehova.
Bado lipo kundi la watu wengine ambao si waislamu wala mashahidi wa Yehova wao pia wanasema:-
1. Utatu ulianzishwa katika Mkutano uliofanyika mji wa Nicea, mwaka 325 B.K Chini ya usimamizi wa mfalme Constantino wa Roma na kuhudhiriwa na maaskofu wapatao 300 toka sehemu mbali mbali duniani .
2. Utatu Mtakatifu ulianzishwa mwaka wa 381 B.k. katika mkutano uliofanyika mji wa Constanti Nipol (kwa sasa ni Napol Italy) chini ya mfalme Theodousius.
3. Wengine wanasema utatu ulianzishwa mwaka 362 B.K. katika mji wa Aleksandiria Misri ambako ulifanyika mkutano wa viongozi wa kawaida.
4. Wengine wanasema fundisho la Utatu lilianzishwa na kasisi Mkatoliki aitwaye Athanasio aliyekufa mwaka 373.B.K.
5. Wengine husema Utatu ni fundisho lililotungwa kusini mwa Ufaransa kwenye karne ya 5 B.K.
6. Wengine wanasema Utatu uliingizwa katika liturgia na baadaye Roma Italy
7. Na waislam siku hizi wanasema Utatu Mtakatifu ni fundisho alilolianzisha Paulo kule Antiokia baada ya Yesu kuondoka.
Huu ni uthibitisho kuwa suala linalohusu Utatu Mtakatifu wanaoumini Wakristo yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kuwa ni kitu kimoja ,huleta shida ya kufahamu.
Tusomapo Biblia inatupa mwanga mzuri kuhusu Mungu.
Sasa tuangalie tunaposema Mungu ni Utatu jambo hilo linaelezekaje kwa yule asiye amini.
Mungu ni wa Utatu yaani Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu , hizi ni nafsi tatu za Mungu Mmoja, na wala siyo miungu mitatu,hizi nafsi tatu ambazo kwa Kiebrania,ambayo ni lugha ya asili iliyotumika katika Agano la Kale huitwa “Elohim” ambalo linaonesha wingi wa Mungu, zinazofanya kazi kwa pamoja na wakati huo huo kila moja ikiwa peke yake (unity in diversity). Hivyo :
UTATU NI MUNGU
1. Baba ni Mungu Fil 1:2 “ Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo”.
• Mwana ni Mungu - Yoh 1:1:14 Kol 2:9
• Hapo mwanzo kulikuwako Neno , naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu ------------, Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba amejaa neema na kweli”
• Kol 2: 9 “ Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa jinsi ya kimwili”.
• Roho Mtakatifu ni Mungu
Mdo 5:3-4 “ Petro akasema Anania kwa nini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uwongo Roho Mtakatifu na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwishauzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako?.Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu”.
N.B.Roho Mtakatifu ni ,nafsi ya tatu ya Mungu yenye hisia “emotion”, huhuzunika (Ef 4:30),hunena, (Uf 2:7), anaweza kuzimishwa ((1Thes 5:19), Hufurahi (Rum 14:17) .Hivyo Roho Mtakatifu ni Mungu Mwenyewe na wala siyo kitu tu (impersonal) (Yoh 4:24) .
Pia katika kitabu cha Isaya 63:7-10 “ Nitautaja wema wa BWANA, Sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israel, aliyowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Maana alisema, hakika ndiyo watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi (Yehoshua) wao. Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia , akawa adui , akapigana nao”
UTATU NI MUUMBAJI2. (a)Nafsi ya Baba. Mwanzo 1:1 “ Hapo mwanzo Mungu (Elohim) aliumba (bara) mbingu na nchi.
Katika mstari huu tunaanza kupata maana ya Utatu. Neno la lugha ya Kiebrania Elohim lenye maana ya Mungu, limesimama kwenye uwingi na neno la Kiebrania bara lenye maana ya “aliumba” limesimama katika umoja.Ingekuwa neno “bara” limeandikwa “barahim” ambalo ni uwingi wa bara ,hapo lingeonesha uwingi na kwa kiswahili lingesomeka “Mungu waliumba” jambo ambalo kamwe Biblia haifundishi hivyo. Maneno hayo hayo ya Kiebrania Elohim na barah yametumika tena katika” Mwanzo 1:26-27.
Isaya 64:8 , “Lakini sasa Ee BWANA, wewe u baba yetu sisi tu udongo, wewe u mfinyanzi wetu ,sisi sote tu kazi ya mikono yako “
Isaya 44:24 “BWANA mkombozi wako yeye aliyekuumba tumboni asema hivi Mimi ni Bwana nifanyaje vitu vyote ,nizitandaye mbingu peke yangu nienezaye nchi ni nani aliye pamoja nami ?”
(a) Mwana Yoh 1:3 Kol 1:15-17
“ Vyote vilifanyika kwa huyo ,wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika “.
Kol 1:15-17”
Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote, kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa , vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyo onekana, ikiwa ni viti vya enzi au usultani au enzi au mamlaka, vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake ,naye amekuwako kabla ya vitu vyote na vitu vyote hushikana katika yeye”
(c) Roho Mtakatifu Ayub 33:4 “ Roho ya Mungu imeniumba na pumzi za Mwenyenzi hunipa uhai”
Ayub 26:13 “Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake-----------------------“
3.UTATU HUFUFUA
(a) BABA: I Thes 1:10 “Na kumngojea mwanawe kutoka mbinguni ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu ,mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja”
(b) MWANA: Yoh 2:19 “Yesu akajibu akawaambia livunjeni Hekelu hili nami katika siku tatu nitalisimamisha “-----------------------
Yoh 10: 17 “ Ndiposa Baba anipenda kwa sababu nautoa uhai wangu ili ni utwae tena
(C) ROHO MTAKATIFU-Rum 8:11
“Lakini ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu , yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho wake anayekaa ndani yenu”
4.UTATU HUKAA NDANI YA WATU
(a) BABA: 2 Kor 6:16
“Tena pana mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu aliye hai, kama Mungu alivyosema ya kwamba nitakaa ndani yao na kati yao nitatembea nami nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu”
(b) MWANA : Kol 1:27
“ ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa nao ni Kristo ndani yenu tumaini la utukufu”
(c) Roho Mtakatifu – Yoh 14:17
“Ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea kwa kuwa haumwoni wala haumtambui: bali ninyi mnamtambua maana anakaa kwenu naye atakuwa ndani yenu.”
5. UTATU UPO MAHALI POTE
(a) Baba: 1Fal 8:27
“Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? tazama mbingu hazikutoshi wala mbingu za mbingu ,sembuse nyumba hii niliyojenga?”
(b) Mwana: Math 28: 19- 20
“Basi enendeni , mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari “
(c) Roho Mtakatifu – Zaburi 139: 7-10
“Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni wewe uko, ningefanya kuzimu kitanda changu wewe uko. Ningekuwa na mbawa za asubuhi na kukaa pande za mwisho za bahari huko nako mkono wako utaniongoza na mkono wako wa kuume utanishika”.
6. UTATU HUJUA YOTE
(a) Baba – 1Yoh 3:20
“Ikiwa mioyo yetu inatuhukumu kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote”
(b) Mwana- Yoh 16; 30
“Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote wala huna haja ya mtu akuulize, kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu”
Yoh 21:17
“Akamwambia mara ya tatu Simoni wa Yohana wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu wanipenda? Akamwambia Bwana wewe wajua yote , wewe umetambua ya kuwa nakupenda, Yesu akamwambia lisha kondoo zangu” (Marko 2:8)
(c) Roho Mtakatifu – 1 Kor 2: 10- 11
“ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu .Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu, ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu ,hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu”
7.UTATU HUTAKASA
(a) Baba – I Thes 5: 23
” “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili ,bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”
(b) Mwana- Ebr 2:10-11
“ Kwa kuwa ilimpasa yeye ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vimekuwepo akileta wana wengi waufikirie utukufu, kumkamilisha Kiongozi Mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso .Maana yeye atakayesema hao wanaotakaswa wote pia wataka kwa mmoja kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake.”
(c) Roho Mtakatifu – 1 Pet 1:
“ Kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu ,Neema na amani na ziongezwe kwenu”
8.UTATU NI MTOA UZIMA
(a) Baba – Mw 2: 7
“ BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi , akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai” Yoh 5: 21 “ Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao”
(b) Mwana- Yoh 5:21
“ maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha vivyo hivyo na mwana huwahuisha wale awatakao”
(c) Roho Mtakatifu –2 Kor 3: 6,8
“ Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa walidumu wa agano jipya , si wa andiko bali wa Roho kwa maana andika huua bali roho huhuisha --------- “ je huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu ?”
9.UTATU NI USHIRIKA
(a) Baba – 1 Yoh 1:3
“ Hilo tuliloliona na kulisikia twawahubiri na nyinyi ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi na ushirika wetu ni pamoja na Baba na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.”
(b) Mwana – I Kor 1:9
“Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa mwanawe Yesu Kristo Bwana wetu”
(c) Roho Mtakatifu – 2 Kor 13:14 “Neema ya Bwana Yesu Kristo na pendo la Mungu na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote”
Filipi 2: 1-2
“Basi ikiwako faraja yoyote katika Kristo yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi ukiwako ushirika wowote wa Roho ikiwako huruma yoyote na rehema, ijalizeni furaha yangu ili mwe na nia moja wenye mapenzi mamoja wenye roho moja mkinia mamoja”
10. UTATU NI WATU MILELE
(a) Baba – Zaburi 90: 2
“ Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia na tangu milele hata milele ndiwe Mungu”
(b) Mwana- Mika 5: 2 , Math 2: 4-6
“Bali wewe Bethlehemu Efrata uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele “ (Math 2:4-6)
(C) Roho Mtakatifu – Ebr 9:14
“Basi si zaidi damu yake Kristo ambaye kwamba kwa roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
11.UTATU UNA UTASHI
(a) Baba – Lk 22: 42
“ Akisema Ee Baba ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki walakini si mapenzi yangu bali yako yatendeke”
(b) Mwana- Lk 22:42
“Akisema Ee Baba ikiwa ni mapenzi yako uniondolee kikombe hiki walakini si mapenzi yangu bali yako yatendeke”
(c) Roho Mtakatifu – I Kor 12:11
“Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye”
12. UTATU HUNENA
(a) Baba – Math 3: 17
“Na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema huyu ni mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye”
(b) Mwana- Lk 5:20 , 7:48
“Naye alipoiona imani yao alimwambia Ee rafiki umesamehewa dhambi zako”
“Kisha alimwambia mwanamke umesamehewa dhambi zako”
(c) Roho Mtakatifu – Mdo 8:29
“Roho akamwambia Filipo ,sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo”
Mdo 11: 11- 12
“ Na tazama mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria, Roho akaniambia nifuatane nao nisione tashwishi.Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami tukaingia katika nyumba ya mtu yule”
Mdo 13:2
“Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga Roho Mtakatifu akasema nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi niliyowaitia”.
13. UTATU NI UPENDO
(a) Baba – Yoh 3:16
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele”
(b) Mwana- Efeso 5:25
“Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa akajitoa kwa ajili yake.”
(C)Roho Mtakatifu – Rum 15:30
“Ndugu zangu nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo wa Roho jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu”
Hoja inayohusu Utatu Mtakatifu iko wazi sana unaposoma Maandiko Matakatifu na ukiyafanya ndiyo dira yako .
Yesu mwenyewe alipokuwa hapa duniani alisema
Yoh 15: 24 “ kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine wasingalikuwa na dhambi ,lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu na kutuchukia “
Swali la ufahamu : Hao watu pale walikuwa wanamuona nani? Baba au Yesu au walikuwa wana muona Yesu ambaye ni Baba? Tafakari.
Katika Yoh 16:13-16
“Lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari zake .Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari .Na yote aliyonayo Baba ni yangu kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu kuwapasheni habari .Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona”.
Swali la ufahamu: Yesu yuko mbinguni na bado tena yuko duniani pote akiwa nani?
Mdo 20:28
“ Jitunzeni nafsi zenu na lile kundi lote nalo ambalo Roho Mtakatifu amewaweka nyinyi kuwa waangalizi ndani yake mpate kulilisha Kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe”
Swali la ufahamu:
“Aliyesulubiwa msalabani ni Mungu,Yesu au Roho Mtakatifu? Bila shaka ni Yesu Kristo”
- Kwanini Kanisa lisiwe mikononi mwa Yesu aliyesulubiwa? Ni kwa sababu Mungu ,Baba,Mwana,na Roho Mtakatifu ni umoja (1 Yoh 5:6-7)
- Mwana amemtukuza Baba duniani (Yoh 17: 4)Baba amewaketisha mwana katika mkutano wake wa kuume wa kiti chake cha enzi mbinguni.
- (Uf 22:1, Marko 16:19)
- Mwana amempa Roho Mtakatifu kazi ya kulitunza kanisa ambalo Mungu alilinunua kwa damu yake.
Ayub 11:7-10
“ Je wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikiria upeo wa huyo mwenyenzi? Ni juu mno kama mbingu waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni kufanya nini wewe cheo chake ni kirefu kuliko dunia ni kipana zaidi ya bahari”.
HASARA YA KUPINGA UTATU MATAKATIFU
Katika I Yoh 2:23
“Kila amkanaye mwana hanaye Baba ,amkiriye mwana anaye Baba pia”
Marko 3:29 “ bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele ila atakuwa na dhambi ya milele”
I Yoh 5:6-7
“ Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu ,Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba na Neno na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja”.Yoh 10:30 ‘ Mimi na Baba tu umoja
SISI NI MALI YA UTATU.
BABA: Yoh 17: 9
“ Mimi nawaombea hao siuombei ulimwengu bali hao ulionipa kwa kuwa hao ni wako”
Mwana: Yoh 17: 6
“Jina lako nimewadhihirishia wale ulionipa katika ulimwengu walikuwa wala ukanipa mimi na neno lako wamelishika.
UTATU NI MWOKOZI
Baba :I Tim 1:1
“Paulo mtume wa kristo Yesu kwa amri ya Mungu mwokozi wetu na kristo Yesu taraja letu”
I Tim 2: 3
“ Hili ni zuri nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu”
I Tim 4: 10
“ Kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili kwa sababu tunatumaini Mungu aliye hai aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wamwaminio”
Mwana : 2 Tim 1:10
“ Na sasa inadhihirishwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu, aliye batili mauti na kuufunua uzima na kutoharibika kwa ile injili.”
Tito 1:4
“ Kwa Tito mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo .Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.”
TUNAUTUMIKIA UTATU
Baba Math 4: 10
“ Ndipo Yesu alipomwambia nenda zako shetani kwa maana imeandikwa msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake”
Mwana: Kol 3: 24
“ Mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi mwamtumikia Bwana Kristo”
TUNAAMINI KATIKA UTATU
Baba : Yoh 14:1
“ Msifadhaike mioyoni mwenu ,mnamwamini Mungu ni aminini na mimi
Mwana: Yoh 14: 1
“Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu niaminini na mimi”
Hivyo Utatu Mtakatifu ambao katika Kiebrania umeelezewa kwa neno la “ELOHIM” hili ndilo fundisho linalomfunua Mungu kihalisi katika Utatu Mtakatifu yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu
Monday, October 11, 2010
FUNDISHO LA UTATU MTAKATIFU: JE NI UPAGANI KAMA WAISLAMU NA MASHAHIDI WA JEHOVA WANAVYODAI? IS TRINITY PAGANISM?
Posted by Unknown on 3:08 AM
5 comments:
MUNGU ALIYE KUJALIA KUONA NA KUNENA HAYA AZIDI KUKUJAZI! in JESUS NAME!
KEEP IT BLUNT! CALL A SPADE A SPADE AND NOT A BIG FOLK!
enlight the true FAITH.
shukuran sana kwa fundisho la utatu mtatakatifu,,,,,ni meelewa sana mwenyezi mung akujalie mwisho mwema
Ndio, UTATU NI UPAGANI, upinge ukatae. Hilo sio fundisho la kimungu na hivi karibuni uchi wa mafundisho hayo nya kipagani ili kuliondoa JINA la mungu utafunuliwa hadharani. HAKUNA ANDIKO LOLOTE LA MOJA KWA MOJA LINALOTAJA UTATU POPOTA. hii ni dhana ya kujitungia.Tumezoea hali za mafundisho mapotovu ya kukanganya kama haya yakijificha kwa biblia baadaye kuanza kuomba pesa. BE AWARE!!!!!!!
1yoh 5; 6-9
imesema utatu mtakatifu, na kama mwalimu alivyoelezea sifa za utatu kuhusu kuumba, kufufua, kuwa mahali popote nk
Mwalimu Daniel, Mungu azidi na kukubariki. Somo umelipeleka vizuri sana.
Post a Comment