Translate

Saturday, November 6, 2010

KWA NINI TATIZO LA UDINI KATIKA SIASA ZA TANZANIA? (THE RELIGIOSITY PROBLEM IN TANZANIA)

HUENDA UNAWEZA KUSHANGAA SANA UNAPOSOMA SWALI LA AINA HII KATIKA BLOGU HII. HAPA TANZANIA TUMESHUHUDIA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KAMPENI ZA KUWANIA UDIWANI, UBUNGE NA URAIS, KAULI MBALIMBALI ZENYE NIA YA KUIONYA JAMII KUHUSU KUTOJITUMBUKIZA KATIKA SIASA ZENYE MLENGO WA KIDINI. LILILONISHANGAZA MIMI, HATA WALE AMBAO NDIYO WAANZILISHI WA KUINGIZA MAMBO YA UDINI KATIKA SIASA ZAO, NAO TUMEWASHUHUDIA WAKIPIGA KELELE KUHUSU UDINI. CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA ILANI YAKE YA UCHAGUZI YA 2005 UK .132 ILIANDIKWA KUHUSU KULIPATIA UFUMBUZI SUALA LA MAHAKAMA YA KADHI ,HUKU KIKIJUA KABISA JAMBO HILO NI LA UDINI KWA MUJIBU WA KATIBA YA TANZANIA IBARA YA 19 i-iv NA 20(i) (a). LAKINI KWA SABABU LENGO LAO LILIKUWA NI KUPATA KURA KUTOKA KWA WAFUASI WA DINI HIYO AMBAYO WAO CCM WALIONA HAWAUNGWI MKONO SANA NALO . CHAMA CHA WANATAALUMA WAKATOLIKI (CPT) WALITOA MWONGOZO WA ELIMU YA URAIA LAKINI BILA KUELEZA NI CHAMA GANI WANACHOKIUNGA MKONO. LAKINI KWA MASIKITIKO MAKUBWA KABISA KAMATI YA SIASA YA SHURA YA MAIMAMU MKOA WA DAR ES SALAAM NA WAO PIA WALITOA 'MWONGOZO' WAO KWA WAPIGA KURA WAO WAISLAMU, AMBAO UNAPOUSOMA UNAWEZA KUSHTUKA SANA ,NA KUKUFANYA USIAMINI UNACHOKISOMA. KWA MFANO KATIKA UK.39-41 WA MWONGOZO HUO KAMATI YA SIASA YA SHURA YA MAIMAMU WANASEMA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA HUU WA 2010 WAISLAMU WANASHIRIKI UCHAGUZI HUU KAMA WAISLAMU NA SIYO KAMA WATANZANIA, NA PIA KUWA UCHAGUZI WA MWAKA HUU KWAO NI IBADA, HUKU MAIMAMU WAKISISITIZWA KUHAKIKISHA JAMBO HILO LINAFANYIKA KWA USAHIHI. SI HAYO TU PIA KAMATI HIYO INASEMA WAISLAMU WAMEWEKEZA NGUVU ZAO KATIKA VYAMA VYA CCM NA CUF . JE WATANZANIA WENGINE WASI WA VYAMA HIVYO WAO WAMCHAGUE NANI IKIWA MGOMBEA SI WA DINI YAO?. NILITEGEMEA SERIKALI INGEKUWA KALI SANA KUHAKIKISHA KUWA MACHAPISHO KAMA HAYO HAYARUHUSIWI KUTOLEWA KATIKA JAMII YETU KAMA KWELI NA WAO HAWAFAIDIKI KWA NAMNA FULANI NA KAMPENI ZA NAMNA HII. HILI LILIJITOKEZA HATA KWA VYOMBO VYA HABARI VYA KIISLAMU HUSUSANI REDIO HERI ILIYOKUWA IKITANGAZA KWA UWAZI KABISA BILA KIFICHO IKIWAHIMIZA WAISLAMU WAMCHAGUE MWISLAMU MWENZAO KIKWETE BILA KUCHUKULIWA HATUA NA TUME YA MAWASILIANO (TCRA) . TUNAAMINI WALISIKIA YOTE.JE WATU WA DINI ZINGINE WALIPOKUWA WANAIONA HALI HIYO NA KUSIKIA KAULI HIZO UNAFIKIRI WANGEKAA KIMYA TU? SIYO RAHISI KWA SABABU IMANI INA NGUVU KULIKO SIASA . TAMBUA HIVYO. HICHO NDICHO CHANZO KIKUU KUHUSU SUALA LA UDINI KUJITOKEZA KWA NGUVU SANA KATIKA KAMPENI ZA MWAKA HUU. NA LIKIACHIWA LIENDELEE MADHARA YAKE NI MAKUBWA KWA TAIFA HILI. SUALA LA TANZANIA KUJIUNGA NA OIC LILILOAHIRISHWA MPAKA MWAKA 2012 NALO INAFAA LIACHIWE WENYE DINI HUSIKA BILA KULIJADILI KWENYE BUNGE LETU LISILO NA DI NI (SECULAR STATE) TAFAKARI!!!!!!!!!!!!!

0 comments:

 
Powered by Blogger