Translate

Monday, May 31, 2010

HONGERA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA (TANZANIA CHRISTIAN FORUM) LAKINI.......

Hatimaye Jukwaa la Wakristo Tanzania, lenye lengo la kuwaunganisha Wakristo wa Madhehebu yote nchini ili yawe na sauti moja, limezinduliwa wiki iliyopita. Jukwa hili linahusisha mabaraza makuu matatu ya Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste (PCT)

Viongozi wetu hao wa Kiroho wanastahili pongezi sana kwa kulifanya jambo hili kuwa halisi. Hii ni kwa sababu kwa kukosekana kwa chombo kama hicho Kanisa limeumizwa sana katika mambo mengi bila kupata muafaka wa haraka.

Mfano makanisa kuchomwa moto bila wahusika kuchukuliwa hatua hata kama si Kanisa la Dhehebu unalotoka wewe m.f Kanisa la EAGT- Fuoni na Bububu, Zanzibar, Wakristo kuwekwa mahabusu kwa sababu eti wamechinja wanyama kwa ajili ya matumizi yao ya chakula badala ya kuwapa Waislamu kuwa ndiyo wanaostahili wawachinjie hata kama hakuna sheria hiyo m.f Mkristo aitwaye Disias Raphael, wa FPCT- Kagunga- Kigoma aliyekamatwa tarehe 26/5/2010 saa 4 kwa kuchinja mnyama wake mbuzi.

Jukwaa hili linatakiwa liwe na uso mgumu mbele ya dola (hard face) katika mambo ya msingi kwa sababu kwa kumbu kumbu zangu ndogo, serikali au dola imekuja baadaye baada ya dini ,hivyo itegemewe kuwa dini iielekeze serikali na dola katika kuhakikisha ustawi wa wananchi wake kwa sababu dini iko karibu zaidi na watu kuliko serikali ambayo inategemea vyombo vyake vya nguvu (coercive tools) kutawala, badala ya upendo.

Hata la siku ya uchaguzi mkuu kupangwa jumapili na Tume mnaweza kulikemea tu na siku ikabadilika mkitaka. Inawezekana.Waislamu wameingiwa na hofu katika jambo hili . Je manajua ni kwa nini Maaskofu wangu? Nitalielezea baadaye. Mungu awabariki

2 comments:

Anonymous said...

Dalili za mwisho.........(kwa wajuao kusoma nyakati)

Anonymous said...

Kuzinduliwa kwa jukwaa la kikristu Tanzania sio jambo baya ili mradi lengo lake liwe ni kuwaunganisha wakristu wote bila kujali ni wakatoriki, wasabato, jehova witnesses au waumini wa father nkwera. Itakuwa ni vibaya tu kama lengo litakuwa la kujitenga na watanzania wengine wasiokuwa wakristu.

Nijuavyo mimi kitendo cha kuchoma moto makanisa kinalaaniwa hata na waislamu wenye kuijua vizuri dini yao na kuitakia mema nchi yao. Naamini pia wakristu wenye kuijua vema dini yao na kuitakia mema nchi yetu hawawezi kufurahia misikiti kuchomwa moto. Kama hivi ndio ndivyo, isingekuwa vibaya hata kama jukwaa lingekuwa la wanadini wote-George Jinasa

 
Powered by Blogger