TAMKO LA WAINJILISTI WA KIKRISTO TANZANIA (UWAKITA)
TAREHE 14 /06/2012 KATIKA UKUMBI WA KANISA LA ST.ALBANO ANGLICAN UPANGA -DAR ES SALAAM
JIHAD YA KUANGAMIZA UKRISTO SASA IMEPAMBA MOTO
Sisi, Umoja wa Wainjilisti wa Kikristo Tanzania (UWAKITA), tumekutana leo kufuatia hali ya machafuko na uchomaji wa Makanisa, vitisho dhidi ya Wakristo na mali zao huko Zanzibar;
Tumekuwa tukitoa matamko ya tahadhari kwa muda mrefu sasa, juu ya matamko yanayotolewa katika makongamano ya Waislamu ambapo kwa kweli tunasikitika kuwa hatukusikilizwa ipasavyo na mamlaka husika.
Tulipofika kwenye awamu ya Pili ya utawala wa Tanzania, palizuka vikundi vya vijana wa Kiislamu. Vikundi hivi vilifanya mikutano ya kuchambua na kukosoa Biblia, kama walivyotaka.
Ilivyoonekana, vikundi hivi viliandaliwa tangu siku nyingi vikisubiri tu atakapokuja Rais Mwislamu waanze kazi ya kuubomoa bomoa Ukristo na kuangamiza Wakristo wenyewe. Sanjari na harakati hizo pakafanyika mipango ya siri ya kuiingiza Zanzibar kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Duniani (O.I.C) na pakatokea mapigo dhidi ya Kanisa kama ifuatavyo:-
HAPA TUNAORODHESHA MATUKIO MACHACHE TU KUTHIBITISHA TUSEMAYO:-
1. MWANZA: Mkristo mmoja akachomewa nguruwe wake kwa moto wa Petrol na mali zake kuharibiwa na Waislamu.
.
2. MAGOMENI:- Mkristo mmoja aitwaye Mbokomu alivunjiwa bucha zake za nguruwe Manzese, huku wavunjaji wakipiga kelele za TAKBIR, wakiwa wamebeba nyundo na mashoka.
3. TANGA:- Kantini ya Kanisa Katoliki ilichomwa moto na Waislamu.
4. KIBAHA:- Kanisa la Kianglikana nalo lilichomwa moto.
5. Mwaka 2002 Kanisa la African Inland (AICT) Pahi Wilayani Kondoa lilichomwa moto na Waislamu na kuteketea.
6. Mwaka 2003 Waislamu walivamia mhadhara wa Wakristo eneo la Kimara Baruti wakitokea msikitini na kuharibu vyombo vya mahubiri hayo. Polisi, lakini hapakuwa na utekelezaji wowote pamoja na kufuatwa mara kwa mara ili wachukue hatua lakini ikawa kimya.
7. Tarehe 9 Novemba 2004, Waislamu wa Namanga kwa kushirikiana na Wasomali kutoka nchi jirani ya Kenya walivamia mkutano wa Injili huko Namanga na kuharibu mali. Jeshi la Polisi halikuchukua hatua yoyote.
8. Mwezi Agosti 2007, Waislamu walivamia na walivuruga ibada ya Jumapili ambayo pia ilihusisha ibada maalumu ya Sakramenti ya Kipaimara iliyokuwa inaendeshwa na Askofu Gerald Mpango wa Kanisa la Kianglikana Dayosisi ya Western Tanganyika huko Nguruka, Kasulu Mkoani Kigoma.
9. Mwaka 2008 Waislamu walivamia mkutano wa Injili huko Kalya wilayani Kigoma Kusini na kuharibu vyombo vya Kanisa vyenye thamani ya Dolla 8,000/=
10. Tarehe 25 Februari, 2011 Waislamu katika mji mdogo wa Mto wa Mbu walivamia mkutano wa Injili na Kuharibu mali za thamani kubwa sana kujeruhi watu na hatimaye kusababisha kifo cha Mwinjilisti, Jackson John wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wilaya ya Monduli, Mto wa Mbu.
11. Tarehe 21 Septemba 2011 kulitokea uchomaji wa makanisa (1)(TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD (T.A.G)-LUMALA PARISH (2)TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD (T.A.G.)-NYAMANOLO PARISH AND (3)PENTECOSTAL ASSEMBLIES OF GOD (P.A.G.)-PASIANSI PARISH, Jijini Mwanza, Uliofanywa na Waislamu.
12. Na hivi karibuni kumezuka tabia ya Jeshi la Polisi kukamata Wakristo wanaochinja wanyama wao wenyewe kinyume cha Sheria kwa shinikizo la Waislamu.
MPANGO WA UCHOMAJI WA MAKANISA ZANZIBAR
Mipango na mikakati ya uchomaji wa Makanisa, iliasisiwa mnamo tarehe 15/01/2011, pale Mashekh wa Zanzibar kwa kushirikiana na Mashekh wa Tanzania bara pamoja na waumini wao, walipokutana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee kupanga kile walicho kiita uzinduzi wa Makongamano ya kupinga Mfumo Kristo.
Makongamano hayo hadi sasa, yamefanyika karibu katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, ukiiacha mikoa hii mipya, iliyotangazwa hivi karibuni na Serikali, kwa lengo la kupandikiza chuki dhidi ya Ukristo.
Katika uzinduzi wa jukwaa la Katiba mmamo tarehe 6/01/2012, Masheikh hao walikutana tena katika ukumbi huo huo ambapo pamoja na mambo mengine waliyo jadiliana, kulikuwa na kauli iliyotoka kwa mmoja wa wakilishi wa Zanzibar, Shekh Azan Khalith aliyesema tunam nukuu. “Sisi kwa upande wetu Zanzibar tunasema kufa kupona Katoliki litang’oka mizizi yake Tanzania. Kwa hivyo nawaambia Waislamu wasiichukulie kauli ya yule kafir mkubwa aliyesema tusichanganye dini na siasa.” mwisho wa kunukuu.
Aliyekuwa mgeni wa Heshima katika uzinduzi wa jukwaa hilo, Sheikh NASORO MOHAMED MAJID akiwashajiisha Wazanzibar alisema: “msiwe na wasiwasi, Waislamu kuna mambo mawili tu kule, ima ziwe Serikali tatu au Muungano umevunjika. Zanzibar kuna kitu ndani yake ndiyo maana inang’ang’aniwa na si kingine isipokuwa ni UKRISTO, ambao wana uhakika Zanzibar ikijing’amua katika huu unaoitwa Muungano, basi Uislamu utapata nguvu, ukishapata nguvu kule, huku Tanganyika maji yanateremka tu.
Basi huo mfumo Kristo ukifanikiwa katika mambo mawili haya yaani (kuung’oa) Basi Waislamu wa Tanganyika tumeshakomboka (kombolewa).” Mwisho wa kunukuu.
Matokeo ya utekelezaji wa kauli hizo ni uchomaji wa Makanisa unaoendelea sasa.
Kwa kauli hiyo hatukubaliani na maneno yanayotolewa na viongozi wa Serikali na watu wengine wenye nia ya kuficha ukweli wa mambo kwa kusema kuwa waliochoma makanisa ni wahuni nawendawazimu.
Uchomaji wa makanisa katika nchi yetu haukuanza tarehe 26 Mei 2012, umekuwepo hadi sasa kwa muda wa miaka 11 huko Zanzibar, na mara zote tumekuwa tukielezwa kuwa wachomaji niwendawazimu. Swali la kujiuliza ni kwa vipi wendawazimu hawa huona Makanisa tu na hawakosei hata siku moja kuchoma misikiti?
Kutumika kwa Jeshi la Polisi katika Jihad ya kuuangamiza Ukristo nchini
Tunaunga mkono tamko la Maaskofu wa Zanzibar la tarehe 30-05-2012 na Tamko la CCT ambapo sehemu kubwa ya masikitiko yao, wameelekeza kwa vyombo vya usalama hasa Jeshi la Polisi, katika tamko hilo wamefichua mambo makubwa ambapo walisema kumekuwa na kauli zinazotolewa na askari Polisi wazawa wa Zanzibar kuwa wataunga mkono vurugu kila zitakapo tokea pia wakabainisha wazi kuwa tangu uchomaji na hujuma mbalimbali kwa Kanisa zilipoanza kutokea, wamekuwa wakivijulisha vyombo vya dola lakini hakuna hatua zozote zilizokwisha chukuliwa.
Kauli hiyo ya Maaskofu inaungwa mkono na Waziri mwenye dhamana na Jeshi la Polisi ( Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) kwa kauli aliyonukuliwa na vyombo vya habari akisema:
“Jumiki imekuwa ikiendesha mihadhara kinyume cha Sheria lakini mikutano yake bado imekuwa ikilindwa na Polisi ili isifanyiwe vurugu na watu wengine. Sikubaliani na vitendo vya Jumiki vya kuchochea uvunjifu wa amani kwa mwaka mzima na nusu huku ikilindwa na Polisi vinginevyo Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo la Tanzania, Said Mwema, na Kamishina Mkuu wake wa Zanzibar Musa Ally Musa, wachukue hatua za kuwajibika wenyewe bila kulazimishwa.”
Kwa kauli hizo hatuoni shaka yoyote kuamini kuwa Jeshi la Polisi linatumika katika Jihad ya kuuangamiza Ukristo.
MAAZIMIO YETU
i Hatuna imani na Jeshi la Polisi kutokana na madhila haya yanayotokea ambayo hayachukuliwi hatua katika wakati muafaka.
ii Tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujenga na kulipa gharama za uharibifu wa mali za Kanisa na za wahanga wengine.
iv Serikali kujibu hoja za Waislamu juu ya MFUMO KRISTO unao lalamikiwa na Waislamu; Kwa kukaa kimya kunawafanya jamii ya Waislamu waamini kuwa madai yao ni sahihi.
v Serikali kuchukua hatua dhidi ya wale wote waliohusika na uchomaji wa Makanisa na uharibifu wa mali; kwani tunaamini wanafahamika. Kutochukuliwa hatua stahiki kuna wafanya wahalifu hao kujiona kana kwamba wao ndio bora kuliko jamii ya watu wengine hapa nchini Tanzania, na hata kufikia hatua ya kujichukulia hatua na kuharibu mali za wasio Waislamu na hata kusababisha madhara ya kifo.
vi Tumefadhaishwa na hotuba ya mheshimwa Rais juu ya matukio ya Zanzibar, hotuba ambayo ilionyesha kuwabembeleza walio sababisha uchomaji wa Makanisa na kuwataka wafanye shughuli zao kwa misingi ya kuanzishwa kwa kundi hilo, sisi tunaamini kuwa kundi hilo halisitahili tena kuitwa kundi halali, ni matumaini yetu kuwa sasa mheshimiwa Rais atatafakari upya na kuchukua hatua sitahiki juu ya kundi hilo.
Vii Tunaitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokuwalazimisha watoto wa Ki-kristo kusoma dini ya Kiislamu mashuleni, na badala yake wapewe haki yao ya kusoma somo la dini yao (ya Kikristo), kama inavyo fanywa kwa Waislamu.
iv Mwisho, sisi kama Wakristo, kwa namna ya pekee tunawaomba Maaskofu, Wachungaji na wengine wote wenye dhamana ya kuliongoza Kanisa la Mungu hapa Tanzania, kuichukua kadhia hii kama changamoto kuwa haya yanayotokea sasa, yanafunua kile kilichoko nyuma ya harakati za Waislamu kuishinikiza Serikali ya Tanzania kujiunga katika O.I.C, na hata ile shauku yao ya kutaka kubadilisha Katiba na sheria za nchi ili kutoa nafasi ya kuundwa Mahakama za Kadhi.
Viongozi wa Kanisa la Tanzania ambao hatuna shaka wanao uelewa mkubwa katika kutafakari na kuchambua mambo, wanalo jukumu na wajibu wa Kitume, Kinabii na Kichungaji, kuwaelimisha Wakristo na wananchi wengine wote wenye mapenzi mema juu ya namna iwapasavyo kuenenda katika misingi ya sheria, haki, imani, na zaidi ya yote katika kumpendeza Mwenyezi Mungu katika mambo yote.
1 comments:
tutaendelea kuhakikisha makanisa hayaoti tena huku zanzibar
Post a Comment